Ijumaa 25 Julai 2025 - 23:22
Wanaochukia Uislamu na wenye ubaguzi wa rangi wamezuia ujenzi wa msikiti nchini Uingereza

Hawza/ Michelle Strogham, mwakilishi wa Chama cha Labour nchini Uingereza, katika hotuba zake amesema kuwa hakupaswi kuwa na nafasi yoyote kwa ubaguzi wa rangi huko Cumbria, na maandamano yaliyoibuka dhidi ya ujenzi wa msikiti yamesababishwa na ukosefu wa uelimishaji sahihi.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, ujenzi wa msikiti huko "Cumbria" ulianza mwezi Januari mwaka huu, na ni muhimu kutaja kuwa kituo hiki cha Kiislamu kitakuwa msikiti wa pekee ndani ya maili hamsini.

"Cumbria" ina jamii kubwa ya Waislamu, na kwa uchache madaktari bingwa wa Kiislamu hamsini wanafanya kazi katika hospitali za umma za eneo hilo.

Michelle Strogham, mwakilishi wa Chama cha Labour nchini Uingereza, pia katika hotuba zake za kampeni ya uchaguzi amesema kuwa hakupaswi kuwa na nafasi kwa ubaguzi wa rangi huko Cumbria, na maandamano yaliyojitokeza dhidi ya ujenzi wa msikiti yametokana na kukosekana kwa uelimishaji.

Paul Jenkins, ambaye ameunda kundi la kupinga maandamano ya kibaguzi katika eneo hilo, alisema: “Upinzani dhidi ya ujenzi wa msikiti siyo msimamo wa watu wote wa Cumbria! Bali ni sauti ya wachache sana wanaojitahidi kulifanya lionekane kubwa, watu wa Cumbria ni watu wa dini na tamaduni mbalimbali, pamoja na tofauti hizi wanapokuwa pamoja, ni chanzo cha fahari kwao, Sisi watu wa Cumbria tunatetea haki ya kujengwa kwa kituo cha Kiislamu hapa.”

Chanzo: Yahoo News

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha